16 October, 2013

WAKAZI WA MBEYA MPO TAYARI !?????????????

                                                  Happy Kamili akiwa katika pozi

Kama wewe ni mkazi wa jiji la mbeya na vitongoji vyake  au ikatokea kuwepo ndani ya jiji hilo siku ya jumapili ya 3/11/2013 basi chukua habari kamili zinzoleta happy,
usikose ndani ya ukumbi wa paradise hotel uliopo soweto jijini mbeya ndipo mahali ambapo watu wote muishio mbeya na vitongoji vyake mnaombwa kukusanyika kuanzia saa 7 mchana kwa ajili ya uzinduzi wa album ya tatu inayokwenda kwa jina la msemaji wa mwisho ni Mungu iliyoimbwa na Muimbaji wa nyimbo za injili anayefahamika kwa jina la Happy Kamili ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa mpango wa Mungu,
huku akisindikizwa na waimbaji kama vile

                                                            Ambele Chapanyota

                                                               Emanuel mgogo

                                                                Martha Baraka
Na wengine wengi mno kama vile Aman Mwasote,Debora mwaisabila........njoo tujumuike pamoja kwa kiingilio cha shilingi 5000 kwa mkubwa na shilingi 1000 kwa mtoo......watu wote mnakaribishwa
KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA 0754625438

17 October, 2012

TINA MAREGO AJA KIVINGINE

  Muimbaji wa nyimbo za injili anayefanya vizuri nje na ndani ya mipaka ya tanzania anayefahamika kwa jina la Tina Marego amesema ya kwamba sasa hivi ameamua kuja kivingine kabisa tofauti na watu walivyomzoea Tina amesema kuwa ameongeza kwa kusema kuwa maishani mwake hakuwahi kuwaza kama atakuja kutoka na style kama hiyo na amesema kuwa hiyo itakuwa na suprise kwa wafuatiliaji wa muziki wa nyimbo za injili
pia amewataka wapenzi wa nyimbo za injili waweze kumpokea kwa ujio wake huo mpya ambao utaambatana na album yake mpya ambayo muda si mrefu kuanzia sasa ataenda kuiachia baada ya kimya kirefu                                             
 

15 October, 2012

WILLIAM NYANGI AFURAHIA MAPOKEZI ALIYOYAPATA NCHINI MAREKANI

Muimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini tanzania ambaye kwa sasa yupo nchini marekani anayefahamika kwa jina la William nyangi amefurahishwa na raia wa nchi marekani kwa mapokezi mazuri waliomfanyia
                                                william nyangi akiwa nje ya nchi
                                               william nyangi akiwa nje
     Ameongeza kuwa licha ya mapokezi aliyoyapata marekani pia amefurahi kutokana na wananchi wa nchini marekani kuzikubali nyimbo zake ususani ya punga mikono ambayo amefanya na mose wa against devil william nyangi atakuwepo nchini marekani mpaka mwezi december mwaka huu kihuduma ya uimbaji
                   
                                                     video ya wimbo wa Baba wewe ni upendo
                                                  wa william nyangi
                     

12 October, 2012

TUKIO KAMILI KATIKA PICHA:MBAGALA ILIVYONUKA LEO, Mabomu kila kona sirahisi vurugu kwisha bila busara kutumika, Mkanisa matatu yavunjwa.

Askari wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani na kuanza kuleta vuru.
 
  
Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani.
   

  
 
Hapa baadhi ya waisilamu walioamua liwalo naliwe nakuamua kuwatunishia msuli polisi nakusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.
 
  
 
 Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira.
   

Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hi
   

Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji 
 
 
 Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi.

Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog
 
 Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waislam eneo la Mbagala Kizuiani wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kufanyiwa dhihaka na mtoto Emmanuel Josephat ambaye aliitem
 
  Polisi wakiwa katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa katika eneo la Mbagala leo
   

Baadhi ya magari yaliyoharibika katika maandamano ya waislam 
 
   

HAMISI SALUM BABA MZAZI WA KIJANA AMBAYE MSAAFU WAKE ULIFANYIWA DHIHAKA NA EMMANUEL JOSEPHAT NA KUZUA MAANDAMANO MAKUBWA YALIYOFANYWA NA WAAISLAMU JIJINI DAR LEO.Picha na Happy Mnale

05 October, 2012

EMMANUEL NA FLORA MBASHA WALIKUWA KAMA MARAISI NCHINI KONGO

 Mwanamuziki Wa Injili wa Nchini Tanzania Flora and Emmanuel Mbasha Safari hii wamekatisha mji wa goma nchini kongo Katika Tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na Watu wengi wakazi wa Goma na Vitongoji vyake. Vilipelekea Jeshi la Congo kuingia Kazini kwa ajili ya Ulinzi wa Wanamuziki hao kila walipokuwa wanakwenda ili kuwaepusha na fujo za furaha za Wakazi wa Congo.

Flora na Emmanuel Mbasha ambao juzi kati wametoka Katika Nchi ya Marekani na Sasa Wako Congo, na baada ya hapo Watakuwa Wakijipanga na Trip zingine za Nje ya Nchi.

Flora na Emmanuel Mbasha ndio Wanamuziki Pekee wa Injili Tanzania ambao wiki chache zilizopita walionesha Moyo wa Shukrani kwa Media za Tanzania kwa Kutambua Mchango wa Vyombo Vya habari Vya Kikristo na Vile Mchanganyiko Maalum.

Big Up Emmanuel na Flora Kwa Kuwakilisha Vema Tanzania.
                              
 
 Watu Nyomiiiii 

 
  Hapa Ndipo walipokuwa wakikaa
Kila wanapokwenda ni Ulinzi
 
watu kibao
 
flora mbasha on the stage
  
ulinzi kila mahali
  
emanuel mbasha akiwa na ulinzi wake mtaani
 
fanya njia fanya njia
 
watu ameniiiiiiiiiiiiiii
 
mwanajeshi huyu uzalendo ulimshinda na kuingia kati
 
ingekuwa bongo dah
 
watu wazidi kubarikiwa kiukweli ilikuwa balaaaaaaa
 

28 September, 2012

DIALO-GAZUKO SIO NDUGU YANGU BALI NI RAFIKI TU

Muimbaji wa nyimbo za injili ambaye anayefuata nyayo za kaka yake[jakson benty] anajulikana kwa jina la Dialo antony kwa sasa anayefanya vizuri na wimbo wake wa 'dunia iko ukingoni' ambayo ameimba kwa style ya rnb amezungumzia suala la watu kumfananisha na muimbaji wa gospel rap gazuko
                                             dialo antony akiwa peke yake
amesema kuwa watu wengi wameshindwa kujua kwamba yeye na gazuko ni marafiki wa kawaida tu nakudhani kuwa ni mapacha kutokana na kufanana amesema yeye alikutana na gazuko mwaka 2010 mwishoni katika studio inayofahamika kwa jina la ndaga records ndipo alipokutana na gazuko na kuanza kufanya huduma pamoja
                gazuko upande kushoto dialo upande kulia wakiwa katika picha ya pamoja   
           kutoka kushoto sir mbezi,dp,wiliam nyangi mwisho gazuko aliyesimama chini ni dialo
                                    UPANDE WA GAZUKO
gazuko naye pia amekiri kutokuwepo kwa undugu kati yao kwa maana dialo kwa baba yake ni mtu wa mwanza na upande wa mama yake ni mtu wa arusha wakati huo gazuko kwa baba yake ni morogoro na kwa mama yake ni sumbawanga kwahiyo watu wasidhani wao kuwa ni mapacha bali udugu wao ni katika kristo tu
                                                        gazuko akiwa peke yake
ameongeza kuwa yeye kwa mara ya kwanza kusikia habari ya dialo ilikuwa mwaka 2010 mwezi wa nane baada ya kutoka nchini burundi aliporudi kwa mara ya kwanza akaambiwa kwamba kuna kijana amefanana naye ameenda kuimba kanisani kwao ila hakufuatilia kwa maana alikuwa na safari ya nchini zambia kwa hiyo alivyorudi kutoka zambia ndipo alipokutana na dialo mwaka 2010 mwisho na ndipo wakaungana na kufanya huduma pamoja huku watu wengi wakidhani ni mapacha lakini si kweli kuwa ni mapacha