
Deouglas Pius a.k.a DP sio jina geni sana kwa wasikilizaji wa 99.20 fm Praise Power radio nawafuatiliaji wa Gospel fleva na Gospel hiphop kutokana na harakati mbalimbali anazozifanya kuupeleka mziki wa injili mbele,Dp ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Power Drive na Muimbaji wa Gospel fleva amefunguka na kusema maisha yake ya ukuaji hayakua ya mepesi kama ilivyokuwa kwa watoto wengine,DP ambaye alikiri kwamba amewahi kuwa mtoto wa mtaani kabisa na kukataa kukaaa katika vituo vya kulelea yatima kuepuka kufanywa mtaji.DP alifunguka vilivyo katiak tamasha la Gospel fleva lilifanyika jumapili ya tarehe 26 august katika kanisa la Mlima wa Mungu Mbezi Beach ambapo tamasha hilo liliwahusisha Wanaharakati wa mtaa,watoto wanaoishi mtaani ambao kwa mujibu wa DP watoto hao ni watoto wa mtaa kabisa ambao walikutwa wakiwa wanaomba tu barabarani au kufanya kazi mbalimbali za mitaani bila kuwa na sehemu ya kuishi,kabla ya kukutana na mdada Ronia Elly kutoka Australia ambaye alikuja Tanzania kufanya field ya mambo yanayohusiana na ustawi wa jamii,ambaye aliwatafutia chumba angalau cha kukaa na kuwafania michakato mingine ya maisha.Kama alivyoeleza DP alikutana na mdada huyo aliyeamua kuwasaidia katika pilika pilika za studio ambao mdada huyo alikua anarekodi na vijana hao ili kuwapa sauti kwenye jamii.DP ambaye alikua mshehereshaji(mc) katika tamasha hilo aliwasisitiza wahudhuriaji wa tamasha hilo kuchangia chochote kwa kununua nakala ya DVD ya watoto hao,akisistiza kwamba hali ya maisha ya mtaani sio nzuri kulingana na yeye mwenyewe ametokea huko huko kwa hiyo anayajua vilivyo..Mnunuaji wa kwanza kabisa wa DVD hiyo alikua ni mwimbaji an]ayesadikika kuwa ni watu wa kwanza kabisa kufanya mziki wa Gospel Hiphop, Pona Hurst Bukuku ambaye pia kwa maelezo ya Mc na yeye mwenyewe pia hata yeye pia aliwahi kukutwa na mikasa ya kuwa mtoto wa mitaan,Pona ambaye uzalendo ulimshinda na kuamua kuinuka mwenyewe na kwenda kuchukua mike angalau kuwaambia machache vijana hao ambapo alisisitiza kuwa Mungu ni zaidi ya serikali,kwa hiyo kama wanataka msaada w

a kweli hawana budi kumgeukia Mungu.Vijana hao ambao wameshafanya audio na video ya mwimbo wao ambao ujumbe mkuu uasema HATUTAKI HURUMA TUNATAKA HUDUMA.Mwisho wa siku ilipangwa mikakati ya kuweza kuwaendeleza sababu mfadhili wa watoto hao Ronia alikua anarudi Australia kwenda kumalizia masomo.
No comments:
Post a Comment