Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania George Aidan Rungu maarufu kama
Rungu La Yesu hivi karibuni amekua moto wa kuotea mbali katika kupeleka
mbele mziki wa injili,Rungu la Yesu ambaye anafanya mziki wa injili wa
injili kwa mahadhi ya kufoka foka au gospel hiphop kama wanavyoita
amekua akifanya harakati hizi kwa muda mrefu lakini kwa kipindi hiki
anaonekana kuongeza cheche vilivyo,wiki mbilii zilizopita Rungu la Yesu
alikua mmoja kati ya wahusika wakuu wa uandaaji wa tamasha la Ze sunday
Of Gospel Hiphop tamasha ambalo lilionekana kuwabariki watu wengii
wanaopenda mziki wa aina hiyo,tulipoongea nae Rungu la Yesu Alikua na
haya ya kusema,"Nachoweza kusema ni kwamba harakati zimepamba
moto,unajua harakati zilikwepo toka kitambo ila kilichofanyika sasa ni
utanuzi wa wigo wa harakati na huduma,kama unavyojua siku hizi kuna wigo
mpana sana katika mitandao ya jamii kutumika kufanyia harakati na ndo
mana watu wanaweza kuona harakati zetu kwa urahisi tofauti na zamani
kabla ya vitu hivi kuwepo,kuhusu tamasha ni kweli tuliandaa tamasha
tarehe 19 ambao waandaji wakuu tulikuaa ni ZE GCRZ,ZE God'z Chosen
Rapperz familia ya mziki ambayo inatujumisha member saba lakini kwa
ajilii ya majukumu mkoani dar es alaam tumebaki member watatu ambao ni
mimi mwenyewe Rungu la Yesu,Sir.Mbezi junior ambae ndiye founder na
Preacher Gazuko,wengine ambao wako mikoani ni Dialo Antony ambae kwa
sasa ki makazi yupo Arusha,Eriki kapinga yuko Songea,Eka injili yuko
masomoni mbeya,Stani boi,na Ben Mayige ambaye kama akikubali atakua
member rasmi wa Ze GCRZ,harakati hazijaishia hapo, kwa sababu bado
tunapanga ratiba za harakati ambapo jumapili ya kwanza ya mwezi wa kumi
tunatarajia kuwepo na tamasha kubwa pia,tumeweka mbali kidogo ili tuweze
ku cope na personal timetable za kila mtu mfano binafsi nina tour
nyingi katikati hapa tuna mkutano wainjili tabora mwezi wa tisa,baada ya
hapo nitaelekea Tanga kisha ntarudi Dar kwa ajili ya tamasha baada ya
hapo nitakua najiandaa na mkutano mwingine pande za mbinga"pia Rungu
alifunguka kuhusu project yake mpya,"kwa sasa hivi siwezi kuiongelea
sana mpaka pale itakapokua tayari ila kwa ufupi namalizia project yangu
ya album pale combimation sounds chini ya man walter ambayo kama
haitabadilika nitaipa jina la Ulokole sio fasheni,kwa sasa nmerelease
track inayoitwa Bwana Yesu asifiwe ambayo pia nimeifanya kwa man
walter".Rungu alikua na hawa wakuwashukuru,"Namshukuru sana Mungu kwa
kunipa kibali katika ulimwengu wa sasa,naishukuru familia yangu,ZE GCRZ
kwa kuwa nami katika harakati,nawashukuru wana gospel hiphop wote ni
wengi kuwataja na kwa upekee nampenda kumshukuru ma bro George Maige kwa
kuni support bila kuwasahau nyie wana habari Mungu awabariki"hivyo
ndivyo Rungu la Yesu alivyofunguka kwa habari zaidi kuhusu yeye na
nyingine nezo nyingi endelea kuwa nasi..