Mwimbaji mashuhuri nchini afrika ya kusini pastor Solly Mahlangu ni mmoja kati ya waimbaji wanaotegemewa kuwasindikiza waimbaji wa kundi la Worship House kutoka jimbo la Limpompo nchini humo watakapokuwa wakizindua CD na DVD yao ya 9 ambayo waliirekodi mapema mwezi huu huko Soweto nchini Afrika ya kusini.
Pastor Mahlangu ambaye ameendelea kujivunia mashabiki kila kukicha kutokana na uimbaji wake pia kujaribu kwake kuimba vionjo kutoka nchi mbalimbali za Afrika kama ilivyo kwa album yake ya ''Mwamba mwamba'' anatarajiwa kufanya mambo makubwa katika uzinduzi huo huku pia mategemeo yakiwa katika wahusika wenyewe ambao wanatarajiwa kufanya vyema hasa ikizingatiwa timu yake imekamilika kwakuwarudisha nyota wake akiwemo Lufuno Dagada.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa State Theatre huko Pretoria tarehe 28 mwezi wa 9
| Lufuno Dagada katika project 3 ya Worship House. |
ZIFAHAMU MBINU ZA ADUI SHETANI (13)--PASTOR ABEL ORGENES
| Pastor Abel Orgenes kiongozi wa huduma ya B'' FAMILY. |
UTANGULIZI:
Kwa kuwa imeandikwa “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” Hosea 4:6a. na pia imeandikwa “Angalia nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza ili kujenga na kupanda”.Yeremia 1:10 na tena imeandikwa “Nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” Mathayo 16:18b.”
Na kwa kuwa sisi ni Jeshi la Bwana Duniani, jeshi la Bwana lazima liwe hodari sababu Bwana tuliye naye ni Shujaa wa vita; na kwamba Jeshi la Bwana lapaswa kuvaa silaha zote na kutambua uwezo wa Silaha zake katika Mungu lakini pia linajua mbinu mbalimbali anazotumia adui shetani, Jeshi ambalo ni Imara tayari kupigana vita vizuri vya Kiroho kwa ushindi mkuu, na kwamba Jeshi la Bwana linatambua kuwa lina kila sababu ya kushinda na zaidi ya kushinda. Yaani Sisi ni zaidi ya washindi. Sasa basi katika mfululizo huu tunaanza kuchambua mbinu za adui kadri roho wa Mungu anavyotujalia.
13 KUKULETEA TAARIFA MBAYA MFULULIZO
Adui wakati mwingine hufanya mashambulizi mfululizo kama alivyofanya kwa Ayubu - Ayubu 1:10 -22. Kabla hujamaliza kutafakari taarifa mbaya uliyoipokea bila breki, mara unasikia msg au simu au mlango unagongwa na mwingine anakuja na taarifa mbaya inayokuhusu wewe au watu wako wa karibu kabla hajamaliza kusema mara simu inaingia yenye taarifa mbaya tena kuhusu mali na vitu vyako nyumbani au kazini au kwenye biashara yako au ya wanaokuhusu.
Wakati mwingine uko kwenye msiba huu mara taarifa nyingine inaingia kuna msiba mwingine mara mwingine mara mwingie tena. Nini matokeo yake? Unajikuta huna muda wa kupanga na kubuni mambo yako unabaki kuahirisha ahirisha, hata kazi ya Mungu unasogeza mbele, huduma unasogeza mbele. Unajikuta pia huna muda wa kusoma neno wala kuomba wala kwenda kwenye Ibada au fellowship. Unajikuta unalalamika na zaidi kumlalamikia Mungu tu na huna muda wa kujibu mashambulizi ya adui kwanza unasahau kabisa kama adui amehusika na zaidi kuchanganyikiwa katika kila jambo na kuzidi kusababisha matatizo na habari mbaya kuzidi.
Unajikuta unatumia pesa na akiba yako zaidi kuliko kuingiza mapato n.k. Unajikuta ukilaumu watu tu kwamba wamekuacha hawakusaidii nk. Dunia imejaa habari mbaya ‘bad news’, yaani ukisikia news basi utasikia mtu mmoja amekufa na wengine kujeruhiwa…mara nyumba imechomwa moto mahali Fulani…mara hili limetokea baya na lile Habari mbaya zina athari sana… Zinaweza kukujengea fikra negative…/ Hata ukitaka kupewa gari utasema ah litapinduka…. Nyumba ah itaungua… Nenda kwa ndege huko unakokwenda ni mbali ah ikianguka? Yesu alikuja kuleta habari njema na sisi tufanyike waeneza habari njema… Mara nyingi tunapoeneza umbea hatuzungumzi mambo mazuri tunazungumza mabaya Vinywa vyetu na vichomwe na moto kama nabii Isaya alivyochomwa… Tubebe habari njema…
Watu wanahitaji habari njema …wamechoka na habari mbaya walizo nazo kila siku… Tena habari njema ikitangulia halafu ikaja neno ‘lakini’ hii lakini inakuwa mmh inaharibu uzuri wote wa habari njema… Afadhali basi habari mbaya ianze halafu ndio useme lakini …lipo tumaini, pamoja na hayo kuna…. Usiangalie au kusikiliza shetani anasema nini Angalia Mungu anasema nini Hebu na mimi nisikukawize nikupe yale ambayo Bwana anasema, ni habari njema za baraka najua unazijua lakini Bwana akupe kukumbuka upya kumbukumbu hii Kumbukumbu la Torati 28 : 1-14. Mstari wa 3 na kuendelea “Utabarikiwa mjini utabarikiwa na mashambani, Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, wadogo wa kondoo zako; Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.Utabarikiwa uingiapo utabarikiwa na utokapo” Mstari wa 7 - Bwana atawafanya adui zako wainukapo juu yako kupigwa mbele yako; watakutokeakwa njia moja; lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
Tafsiri ya kiingereza inaonyesha kuwa adui watabigwa si mbele yako tu mbele ya uso wako “The LORD shall cause thine enemies that rise up against thee to be smitten before thy face: they shall come out against thee one way, and flee before thee seven ways.” Sababu ya Huduma yetu kuwa na Neno Blessed ni kukumbuka kuhusu baraka tulizoahidiwa, kwa kiingereza mstari wa 3 ungesomeka hivi ‘B’lessed shalt thou be in the city, and blessed shalt thou be in the field. na pengine ungeniuliza sasa mwalimu mbona katika jina la huduma hakuna jeshi hakuna vita Sasa ngoja nichambue hapa; neno ‘B’orn Again ni kutangaza vita na shetani sababu unaachana naye na kuingia katika familia ya Mungu, sasa na hii familia ya Mungu Imebarikiwa na sasa neno jeshi au vita linakuwa kwenye mstari wa 7 hapo juu kwamba sehemu ya baraka ni ushindi dhidi ya adui zetu.
Kwa hiyo kuna kutangaza vita halafu adui akiinuka habari njema ni kwamba atapigwa vibaya sana. Mstari wa nane ni muhimu pia sababu unatukumbusha tarehe tuliyoanza huduma yetu tarehe 8 mwezi wa 8 sasa hebu tuone unasemaje “Bwana ataiamuru ‘B’araka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako”. Sasa ghala ni sehemu ya kuhifadhi chakula unachovuna, ambapo katika Dunia ya leo ghala inakuwa ni kilelezo cha sehemu ya kuhifadhi Fedha zako unazovuna.
Kwa hiyo account yako itabarikiwa na hii itasababisha na Benki yako ibarikiwe. Biblia yasema nini kuhusu habari ? Zaburi 112:7 Hataogopa habari mbaya, moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. Sasa huyu mtu ambaye moyo wake u imara na kwamba hataogopa habari mbaya ni mtu wa namna gani? Je twaweza kuwa kama yeye? Ili kuelewa ni mtu wa namna gani lazima tusome Zaburi 112 tangu mwanzo , sasa tuanze mstari wa kwanza unaanza kama ifuatavyo “Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.
Wazao wake watukuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Heri atendaye fadhili na kukopesha ; atengenezaye mambo yake kwa haki. Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. Mtu ambaye hataogopa habari mbaya ni yule
o Amchaye Bwana
o Apendezwaye na maagizo ya Bwana
o Muadilifu
o Aliyebarikiwa
o Mwenye haki
o Mwenye fadhili
o Imara na
o Anayemtumaini Bwana wakati wote maishani mwake.
Huduma ya ‘B’ familiy imelenga kukutengeneza uwe mtu wa namna hiyo. Lakini pia tunaona katika Mithali 25:25 ni rahisi kuishika hii mithali 25: 25 inasema “Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu, Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali”.
‘B’ Family imelenga ku challenge watu wake kwenda mbali kupeleka habari njema, kwenda mbali nje ya miji – vijijini, milimani na mabondeni lakini pia kwenda mbali nje ya Tanzania kokote ulimwenguni kuliko na watu wenye kiu.
Lakini pia tutatumia tecknolojia kuwafikiwa mtu yeyote aliyembali kwa habari njema. Na katika Isaya 52:7 imeandikwa “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye Amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki! Sasa huyu shetani anayeleta taarifa mbaya, habari mbaya ni sawa na kusema hivi juu yake na wale anaowatuma kwamba Jinsi ilivyo mibaya juu ya milima miguu yake yeye aletaye habari mbaya na kuendelea… Mambo mengine ya kufanya katika kushinda mbinu hii ya adui yanahusiana moja kwa moja na Maisha ya Imani.
o Simama katika NENO na ahadi za Mungu kwa Imani.
o Usiangalie au kusikiliza shetani anasema nini juu yako Angalia Mungu anasema nini juu yako na amini anayosema.
o Tunaishi kwa Imani kwa kusikia na kutii Neno na Imani yetu inatenda, inaleta matokeo, na Mungu anafanya kazi na watu wake kwa njia ya imani.
o Haijalishi hali ni mabaya namna gani ipo ajira nzuri kwa mtoto wa Mungu kwa nini? Kwa sababu hiyo ndio Imani na Imani yetu ina Nguvu kushinda ulimwengu.
o Yako mafanikio na Baraka tele kwa kila aaminiye kwa hiyo ndugu yangu Amini Neno, na endelea kuamini katika Mungu kwa maisha yako ya kawaida yaani Ishi kwa Imani. Na maisha ya Imani humpendeza sana Mungu. Familia ya Mungu duniani ni familia ya Imani inayoishi kwa Imani.
o Tunaweza kubatilisha Taarifa mbaya kwa Imani katika Jina la Yesu, hasa zinazohusu maisha yajayo, Adui anapokwambia wewe ni maskini na utakufa maskini – Sema nakataa hilo kwa jina la Yesu, Nina Baba Tajiri, na utajiri wangu unaanza Rohoni yaani Uzima wa milele na uweza na mamlaka na katika Nafsi, utajiri wa Amani, Furaha, Upendo, Utu wema, Uaminifu na Mwilini Afya, Kibali, na mahitaji yangu yote yanashughulikiwa na Mungu wangu kila siku.
Somo litaendelea Ijumaa ijayo....
NB: Mungu akubariki kwa kupata nakala ya mafundisho haya, hizi ni baadhi ya mbinu za adui kati ya mbinu zaidi ya 100 ambazo zimeandikwa....NA PIA MAFUNDISHO HAYA YAKO KATIKA CD ya kusikiliza....na karibu sana katika kituo cha mafundisho: Bounty Beach Resort, Mji mwema, Kigamboni, kwa daladala kituo ni REDPOT/mbuyuni. Tunakutana kila jumapili kuanzia saa 9 mchana. Kwa mawasiliano zaidi: Facebook: Abel Orgenes - 0715 94 222 1 Email : abelorgenes@yahoo.com Simu : Rebecca Orgenes - +255 715 928 433 Dar es Salaam, Tanzania.
Thursday, 30 August 2012
KWA TAARIFA YAKO--ZIFAHAMU KWAYA ALIKOANZIA ROSE MUHANDO
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
Katika KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kuhusu mwimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando ambaye ameanza kupata umaarufu nchini na nje ya nchi tangu atoe kanda yake ya kwanza iitwayo ''Mteule uwe macho'' yenye nyimbo nzuri mbalimbali, lakini kabla ya hapo mwimbaji huyu alianzia kwenye kwaya mbalimbali akiwa kama mwalimu pia mwimbaji kati ya kwaya ambazo GK inazijua ni Mamajusi kutoka kanisa la Anglican St. Margaret Majengo mjini moshi mkoani Kilimanjaro ambako mwimbaji huyu alifanya vizuri sana kwa kurekodi nyimbo mbalimbali na kwaya hiyo.
Kati ya nyimbo ambazo unaweza kusikia sauti yake vyema ni pamoja na Hey Haleluyah, Homa ya dunia( ambao ukiusikia sauti umeshabihiana na wimbo wake mteule uwe macho) na nyimbo nyinginezo, ukiacha kwaya hiyo mwimbaji huyo pia aliifundisha kwaya ya Sifuni kutoka kanisa la Kilutheri mkoani Morogoro ambako aliweza kuifundisha vyema kwaya hiyo hatimaye ilifikia wakati wa kurekodi album lakini kuna mambo yaliyokuwa yamejitokeza hivyo mwimbaji huyo kutorekodi na kuelekea mkoani Dodoma lakini nyuma yake kwaya hiyo ilirekodi wimbo kama Mteule uwe macho ambao ulipaswa uanzishwe na Rose mwenyewe lakini kwaya hiyo ikampa mwimbaji mwingine kuanzisha ambaye pia aliweza kujaribu vyema.
Kwa upande wa Rose yeye alipokwenda mkoani Dodoma ndipo alipoamua kutoka kama mwimbaji binafsi na kutoa album yake ya Mteule uwe macho pia akiwa mwalimu na mwimbaji wa kwaya ya Anglican St. Mary Chimuli ambao nao kupitia Rose Muhando waliweza kutoka vyema kwa album yao iitwayo Kitimutimu iliyokuwa na nyimbo mbalimbali zikiwemo zilizotungwa na kuanzishwa na Rose Muhando mwenyewe ingawa hakuweza kudumu na kwaya hiyo kutokana na mambo yaliyojitokeza hivyo kuamua kuanzisha kundi nje ya kanisa ambalo analompaka sasa akiwa amefanikiwa sana.
ANGALIA NYIMBO AMBAZO ZINA SAUTI YA ROSE MUHANDO AKIANZISHA, LAKINI KWAKUWA ALISHATOKA WAIMBAJI WENGINE WAKAIGIZA KWENYE VIDEO, LAKINI ALIYEIMBA NI ROSE MUHANDO.
HAPA MCHEKI ROSE MUHANDO AKIWA NA KWAYA YA KITIMTIMU ST. MARY CHIMULI DODOMA ANGLICAN AKIIMBA NAJITOA SASA.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama ulikuwa hujui vinginevyo tukutane wiki ijayo.
| Rose Muhando. |
Katika KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kuhusu mwimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini bibie Rose Muhando ambaye ameanza kupata umaarufu nchini na nje ya nchi tangu atoe kanda yake ya kwanza iitwayo ''Mteule uwe macho'' yenye nyimbo nzuri mbalimbali, lakini kabla ya hapo mwimbaji huyu alianzia kwenye kwaya mbalimbali akiwa kama mwalimu pia mwimbaji kati ya kwaya ambazo GK inazijua ni Mamajusi kutoka kanisa la Anglican St. Margaret Majengo mjini moshi mkoani Kilimanjaro ambako mwimbaji huyu alifanya vizuri sana kwa kurekodi nyimbo mbalimbali na kwaya hiyo.
Kati ya nyimbo ambazo unaweza kusikia sauti yake vyema ni pamoja na Hey Haleluyah, Homa ya dunia( ambao ukiusikia sauti umeshabihiana na wimbo wake mteule uwe macho) na nyimbo nyinginezo, ukiacha kwaya hiyo mwimbaji huyo pia aliifundisha kwaya ya Sifuni kutoka kanisa la Kilutheri mkoani Morogoro ambako aliweza kuifundisha vyema kwaya hiyo hatimaye ilifikia wakati wa kurekodi album lakini kuna mambo yaliyokuwa yamejitokeza hivyo mwimbaji huyo kutorekodi na kuelekea mkoani Dodoma lakini nyuma yake kwaya hiyo ilirekodi wimbo kama Mteule uwe macho ambao ulipaswa uanzishwe na Rose mwenyewe lakini kwaya hiyo ikampa mwimbaji mwingine kuanzisha ambaye pia aliweza kujaribu vyema.
Kwa upande wa Rose yeye alipokwenda mkoani Dodoma ndipo alipoamua kutoka kama mwimbaji binafsi na kutoa album yake ya Mteule uwe macho pia akiwa mwalimu na mwimbaji wa kwaya ya Anglican St. Mary Chimuli ambao nao kupitia Rose Muhando waliweza kutoka vyema kwa album yao iitwayo Kitimutimu iliyokuwa na nyimbo mbalimbali zikiwemo zilizotungwa na kuanzishwa na Rose Muhando mwenyewe ingawa hakuweza kudumu na kwaya hiyo kutokana na mambo yaliyojitokeza hivyo kuamua kuanzisha kundi nje ya kanisa ambalo analompaka sasa akiwa amefanikiwa sana.
ANGALIA NYIMBO AMBAZO ZINA SAUTI YA ROSE MUHANDO AKIANZISHA, LAKINI KWAKUWA ALISHATOKA WAIMBAJI WENGINE WAKAIGIZA KWENYE VIDEO, LAKINI ALIYEIMBA NI ROSE MUHANDO.
HAPA MCHEKI ROSE MUHANDO AKIWA NA KWAYA YA KITIMTIMU ST. MARY CHIMULI DODOMA ANGLICAN AKIIMBA NAJITOA SASA.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama ulikuwa hujui vinginevyo tukutane wiki ijayo.
KURASINI SDA CHOIR KUTOA ZAWADI MAALUMU JUMAMOSI HII
| Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Kurasini SDA katika moja ya huduma. |
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kwaya hiyo zinasema kwamba siku ya jumamosi itakuwa ''KWAYA DAY'' ambapo nyimbo mbalimbali za zamani zikiwemo za harusi na nyinginezo zitaimbwa na kwaya hiyo katika tukio ambalo litafanyika kanisani kwao Kurasini nyuma ya viwanja vya maonyesho vya mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba.
Kwaya hiyo ambayo GK inathubutu kusema kwamba ni moja kati ya kwaya bora kabisa kwa uimbaji nchini mpaka sasa ina album zaidi ya 35 ikiwa chini ya walimu mbalimbali akiwemo Samson Kibaso ambaye anasifika kwa ufundishaji wake katika kwaya mbalimbali ndani na nje ya nchi, pia sifa nyingine ya kwaya hii ni aina ya nyimbo inazoimba zimekuwa zikitajwa kubariki na kuokoa maisha ya watu wengi hadi kusababisha kupata mialiko kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Ambapo siku ya jumamosi hakutakuwa na kiingilio katika tukio hilo, zaidi kwaya hiyo imeahidi kushusha uwepo wa Mungu kwa nyimbo mbalimbali kuanzia katika ibada asubuhi hadi jioni ilimradi watu wapate mda mzuri wa kusikiliza nyimbo kutoka katika kwaya hiyo pamoja na kwaya alikwa kama Kinondoni SDA, Ubungo Hills SDA, Magomeni SDA pamoja na Miriam Sassi na Joseph Oola.
HAPA WACHEKI KATIKA MOJA YA VIDEO ZAO WIMBO ''JERUSALEM'' NA ''BADO
No comments:
Post a Comment